BREAKING NEWS

Comments

Wednesday, November 15, 2017

Chanzo cha Kifo cha Hamad Ndikumana


Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Timu ya Soka ya Rayon Sports nchini Rwanda, Hamad Ndikumana Katauti amefariki dunia ghafla leo hii. Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Rayon Sports Gakwaya Olivier, amesema muda mfupi uliopita kwamba kifo cha Ndikumana kilisababishwa na ugonjwa wa moyo.
“Alisikia maumivu makali kifuani akaomba soda ya baridi wakamletea na alipomaliza kunywa tu kidogo akatapika na akaishiwa pumzi na ndipo akakata kauli,” alisema Olivier na kuongeza kwamba bado wanasubiri uchunguzi wa madaktari.
Ndikumana ambaye amewahi kucheza soka Tanzania akiwa na klabu ya Stand United, amewahi kuwa mume wa muigizaji Irene Uwoya na wana mtoto mmoja.

Share this:

Post a Comment

 
Back To Top
Copyright © 2014 JAMII FOCUS. Designed by OddThemes