Mshambuliaji wa Young Africans , Obrey Chirwa amechaguliwa kuwa Mchezaji bora wa Oktoba wa Ligi Kuu ya ya Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2017/2018.

Kiwango cha mchezaji huyo kilionekana pia katika mchezo wa watani wa jadi Yanga na Simba uliofanyika Oktoba 28, 2017 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1. bao la Yanga lilifungwa
na Chirwa.
na Chirwa.
Chirwa raia wa Zambia alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, beki Erasto Nyoni wa Simba na mshambuliaji Ibrahim Ajib pia wa Yanga alioingia nao fainali katika uchambuzi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za VPL zinazotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
Post a Comment