BREAKING NEWS

Comments

Friday, November 10, 2017

Diamond ambwaga Hamisa Mabeto


Mwanamitindo Hamisa Mabeto amekwaa
kisiki mbele ya Diamond Platnumz baada ya
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande
wa Watoto kutupilia mbali kesi
aliyomfunguliwa mwanamuziki huyo juu ya
matunzo ya mtoto Prince Abdul.
Uamuzi huo umetolewa leo Ijumaa na Hakimu
Devotha Kisoka wa Mahakama hiyo baada ya
kusikiliza hoja za pande hizo mbili husika.
Diamond aliwasilisha pingamizi dhidi ya kesi
hiyo iliyofunguliwa na Mobeto akidai kuwa
kesi hiyo imefunguliwa kwa kutumia kifungu
ambacho si sahihi. Hoja ambayo ilipingwa na
Mobeto.
Mobeto alifungua kesi hiyo mahakamani
hapo, pamoja na mambo mengine anaiomba
matunzo ya mtoto waliozaa na msanii
Diamond.
Mobeto anaiomba mahakama imwamuru
Diamond kutoa matunzo ya mtoto ya kila
mwezi na alifungua kesi hiyo kupitia
mawakili wake Abdullah Lyana na Walter
Godluck kutoka kampuni ya uwakili ya
Century Attorneys.
Kupitia hati hiyo ya madai, Mobeto anaomba
Diamond amuombe msamaha kwa
kumsababishia madhara yaliyoishtua familia
yake.
Diamond aliwasilisha hati ya majibu hayo
kinzani akipinga maombi hayo ya Mobeto
akidai gharama anazodai kulipwa kwa mwezi
ya Sh5 milioni kwa ajili ya matunzo ya mtoto
ni kubwa hawezi kuzimudu.

Share this:

Post a Comment

 
Back To Top
Copyright © 2014 JAMII FOCUS. Designed by OddThemes