BREAKING NEWS

Comments

Wednesday, November 22, 2017

Kikosi cha Simba SC chaendelea na mazoezi makali kuikabili Lipuli FC

Kikosi cha Simba SC hii leo kimeendelea na mazoezi katika viwanja vya polisi, jijini Dar es salaam.
Simba ambayo imeanza mazoezi yake hapo jana siku ya Jumanne baada ya kutoka katika mapumziko mafupi baada ya mchezo dhidi ya Tanzania Prisons wiki iliyopita.
Kikosi cha Simba kinajipanga kuelekea mchezo wake wa siku ya Jumapili dhidi ya Lipuli FC ya Iringa, mchezo ambao awali ulipangwa kupigwa pale Uwanja wa Uhuru kabla ya mabadiliko ambapo sasa utachezwa katika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, jijini Dar es Salaam.

Share this:

Post a Comment

 
Back To Top
Copyright © 2014 JAMII FOCUS. Designed by OddThemes