Beki wa kati Phil Jones alilazimika kutomaliza mchezo wa timu yake ya taifa ya England baada ya kuumia wakati ilipokuwa ikikipiga dhidi ya Ujerumani, jana katika mchezo wa kirafiki.
Kuumia kwa beki huyo kunaweza kuongeza pigo kwa Manchester United chini ya Kocha Jose Mourinho.
Mourinho amekuwa na wachezaji kadhaa majeruhi akiwemo straika mkongwe Zlatan Ibrahimovic ambaye yupo njiani kurejea uwanjani kutoka katika majeraha ya goti.
Phil Jones aliumia katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Wembley ikiwa ni mchezo wa kirafiki.
Jones alianza kuchechemea kuanzia katika dakika ya 10 lakini baadaye aliendelea hadi dakika ya 24 alipotoka.
Post a Comment