BREAKING NEWS

Comments

Wednesday, November 8, 2017

Mwanafunzi aliyedaiwa kufa yuko ICU


Kamanda wa  Polisi mkoani Kagera Agustino Ollomi amewataja majina wanafunzi ambao wamefariki dunia kutokana na bomula  kutupwa kwa mkono katika shule ya msingi Kihinga wilaya ya Ngara mkoani Kagera.Kamanda Ollomi amesema kwamba wanafunzi hao ni Juliana Tarasisi (13) Evart Theonas (12) Edson Bigilimana (12), Miburo Gabriel (12), na Tumsifu Ruvugo (8).Pia Kamanda huyo amesema mtoto wa sita aliyedhani amefariki alibainika kuwa bado yuko hai na yuko mahututi kwenye chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU).Amesema  mwalimu wa darasa, Policalipo Clemency aliyekuwa darasani wakati wa tukio ni miongonimwa waliojeruhiwa na kulazwa hospitali.Akizungumzia tukio hilo, Mwalimu Clemency amesema  wakati bomu linaipuka, alikuwa akiandika mtihani wa kusoma ubaoni na kila mwanafunzi alikuwa akiingia na kusoma ili kumwekea alama kwa ajili ya mitihani ya kufunga mwaka.“Ghafla nilisikia kishindo kikubwa nakuona baadhi ya wanafunzi wakianguka, walipoteza fahamu na wengine kutokwa damu,” amesema ClemencyMmoja wa wazazi aliyepoteza mtoto katika tukio hilo, Bigimana Kaloli amesema baada ya kusikia kishindo alikimbilia shuleni na kusikia mtoto wake anayeitwa  Edson akiwa tayari amefariki na kusema jambo hilo limeipa familia yake simanzi kubwa.

Share this:

Post a Comment

 
Back To Top
Copyright © 2014 JAMII FOCUS. Designed by OddThemes