BREAKING NEWS

Comments

Saturday, November 11, 2017

TAWA, Polisi wakamata jangili, meno ya Tembo

Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro kwa kushirikiana na Maafisa wa Uhifadhi wa Wanyamapori wamefanikiwa kumkamata jangili akiwa na meno ya Tembo 5 yenye thamani ya MIL 100 na mshitakiwa yuko kituo cha Polisi morogoro.

Taarifa kutoka kwa jeshi la Polisi morogoro mshtakiwa anategemea kufikishwa mahakamani. Aidha, Afisa Habari wa Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania – TAWA Bw. Twaha Twaibu ameeleza kuwa walipata taarifa kutoka kwa raia wema juu ya kuwepo kwa jangili huyo wa meno na kutuma maafisa wanyamapori kutoka Makao Makuu ya TAWA wakishirikiana na jeshi la Polisi na kuweza kumkamata jangili huyo.

Nae Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Ulrich Matei akiongelea tukio hilo, amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo aliejulikana kwa jina la Nehemiah Nashon akiwa katika chumba namba 104 cha Hoteli ya BZ iliyopo maeneo ya Nane-nane Mjini Morogoro, na kwamba vipande hivyo vina thamani ya zaidi ya shilingi Mil. 100.

Share this:

Post a Comment

 
Back To Top
Copyright © 2014 JAMII FOCUS. Designed by OddThemes