BREAKING NEWS

Comments

Entertainment

Fashion

?max-results="+numposts2+"&orderby=published&alt=json-in-script&callback=recentarticles2\"><\/script>");

Food

Thursday, November 30, 2017

Watu 6 washikiliwa kwa kukutwa na mifupa ya albino, ulimi wa simba

Watu sita wanashikiliwa na polisi mkoani Songwe kwa tuhuma za kukutwa na vipande vitatu vya mifupa ya mtu wanayedai kuwa ni albino, pamoja na mafuta na ulimi unaodhaniwa kuwa wa simba.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Mathias Nyange alisema jana kuwa watu hao walikamatwa juzi saa 7:00 mchana katika mji wa Tunduma wilayani Momba na askari waliokuwa doria.

Alisema watuhumiwa hao walikutwa na mafuta ya simba, mifupa mitatu ya albino, mfupa mmoja wa mnyama ambaye hajajulikana, na vipande viwili vya ulimi, vitu vinavyosadikiwa kuwa ni vifaa vya tiba asili.

Kamanda Nyange alidai kuwa baada ya kuhojiwa, watuhumiwa walikiri kuwa mifupa waliyokutwa nayo ni ya albino waliyemkata mkono mkoani Morogoro.

Alisema kati ya watuhumiwa hao wawili ni wakazi wa Morogoro, wawili wakazi wa Mbozi, mmoja ni mkazi wa Wilaya ya Momba na mwingine ni kutoka Nakonde nchini Zambia.

Nyange alisema watuhumiwa hao wanatarajia kupelekwa mkoani Morogoro ambako ndiko wanakotuhumiwa kutenda kosa.

Wakati huohuo, Nyange amesema watu watatu wanaokadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25 na 30 wamefariki dunia baada ya kupigwa risasi na askari waliokuwa doria saa 4:00 usiku wa Novemba 30 baada ya kukaidi amri ya kusimama ya polisi ambao waliwatilia shaka.

Baada ya kukataa kutii amri ya kusimama, polisi waliwafuatilia na baadaye watu hao walianza kuwafyatulia risasi, jambo ambalo kamanda huyo alisema liliwalazimisha askari kuanza kujibizana nao.

Alisema baada ya kuwapekua walikutwa na silaha moja aina ya bastola iliyotengenezwa kienyeji inayotumia risasi za short gun ikiwa na risasi moja na pia walikutwa na mapanga mawili pamoja na kipande kimoja cha nondo.

Magazeti ya Leo Ijumaa ya Decemba 1


Waziri Mbarawa Atoa Maagizo Mazito Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amesema anasikitishwa na utendaji wa Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), kutofanya maamuzi kwa wakati hali ambayo inachangia malalamiko kuongezeka Bandarini hapo.

Aidha, Mbarawa amesema Serikali inapeleka Naibu Mtendaji Mkuu mpya wa shughuli za Uendeshaji Bandarini hapo kutokana na aliyekuwepo kushindwa kusimamia majukumu yake ipasavyo.

Profesa Mbarawa amesema hayo leo wakati wa ziara ya kushtukiza aliyoifanya bandarini ikiwa ni siku chache baada ya Rais John Magufuli, na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kufanya ziara ya kustukiza na kubaini madudu bandarini hapo.

Ziara ya Waziri Mbarawa ni mwendelezo wa ziara mbalimbali bandarini hapo  kubaini uendeshaji na utendaji wa shughuli zinazotolewa na Mamlaka hiyo.

“Nimelazimika leo kuwaita Watendaji na Bodi ya TPA ili kuwaeleza kasoro zenu  ambapo inaonesha wazi kuwa  asilimia kubwa ya mambo yanayotokea humu  ni  kuwa mnakuwa wazito katika kutoa  maamuzi”, amesema Profesa Mbarawa.

Amesema katika bandari hiyo ipo mizigo ya kahawa ambayo imefika bandarini tangu mwaka 2014 huku kukiwa hakuna sababu za kueleweka za wenye mali kutochukuwa mizigo yao.

Profesa Mbarawa amesema hahitaji wasaidizi ambao wanakaa katika vikao na kulipana posho ila wanapaswa kufanya kazi ya kuangalia shughuli zote za bandari.

“Kama hamtabadilika nitaendelea kuja katika bandari hii ili kuchukua hatua pale ambapo inaonekana kwani haipendezi kila kukicha malalamiko kutokea,” amesisitiza Waziri Mbarawa.

Aidha, Waziri Mbarawa ameitka bodi na menejimenti kuhakikisha kuwa inatatua changamoto iliyopo katika bandari ya kushusha na kupakia mizigo kutoka Zanzibar na kuingia Tanzania Bara ambapo wafanyabiashara wanalalamikia utaratibu unaotumika kuwahudumia.

Amesema haingii akilini kuona mizigo inayotoka au kwenda Zanzibar kutozwa kodi baada ya masaa huku inayotoka nje ya Tanzania ikitozwa baada ya siku saba.

Kuhusu ujio wa Naibu mtendaji Mkuu mpya Mbarawa aliitaka Bodi na menejimenti kumpa ushirikiano ili aweze kutoa matokeo chanya kwenye bandari.

“Tunaleta Naibu Mtendaji Mkuu mpya ambaye atasimamia operesheni, naomba apewe ushirikiano ili kusaidia Serikali huyu ambaye anakaimu tunamuondoa ameshindwa kwenda na kasi yetu,” amefafanua Profesa Mbarawa.

Akizungumza baada ya ziara hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya TPA Ignas Rugaratuka, amesema wamejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa wanaitendea haki nafasi waliyopewa kwa kusimamia mabadiliko ndani ya bandari.
Amesema tangu waingie wamekuwa wakipambana kuhakikisha kuwa mapungufu ya TPA yanaisha ambapo wamefanikiwa kurekebisha kwenye utawala kwa kutoa mafunzo kwa watumishi na kuzuia wizi ambao ulikuwa umekithiri.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko, amesema kuwa tangu aingie katika mamlaka hiyo wamekuwa wakifanya jitihada za kurekebisha mapungufu na kumuahidi waziri kuwa ataongeza jitihada zaidi.

“Kama ni mabadiliko tumefanya makubwa sana hasa katika utawala na uongozi ila kila anayehusika katika sekta hiyo anapaswa kutoa msaada,” amesema Mkurugenzi Mkuu.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Finland Yaipiga Jeki Tanzania Shiingi Bilioni 75 Kuendeleza Ubunifu, Misitu Na Uongozi Bora

Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
Serikali ya Tanzania na Finland zimetiliana saini mikataba mitatu yenye thamani ya Euro milioni 28.8 sawa na Shilingi bilioni 75 kwa ajili ya kuendeleza misitu, ubunifu na masuala ya uongozi.

Akizungumza wakati wa utiaji saini wa mikataba hiyo, Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James amesema, msaada huo kutoka Finland umetolewa ili kuendeleza  uwezo wa viongozi na kufanya maamuzi sahihi yenye tija kwa ukuaji wa uchumi wa Taifa, mradi ambao unasimamiwa na Taasisi ya Uongozi, ambapo kiasi cha Euro milioni 9.90 zimetolewa kuendeleza mradi huo.

Aidha Serikali ya Finland imetoa kiasi cha Euro milioni 8.95 kwa mradi wa  kuiimarisha mfumo wa ubunifu nchini kwa kutengeneza mazingira rafiki kwa wabunifu ili kuweza kubuni na kuendeleza ubunifu wao na kuchochea ukuaji wa viwanda.

Bw. James alisema fedha hizo zitatumika kuwasaidia wabunifu kwa kuwapatia vifaa na msaada wa kitaalamu ili kuyaendeleza mawazo yao na kuyafanya yawe ya kibiashara na kuweza kusaidia kubadili mawazo hayo kuwa viwanda.

“Fedha hizi zitasaidia kutatua changamoto katika viwanda vilivyopo nchini ili vifanye kazi kwa ufanisi kwa kuwaunganisha wanataaluma mbalimbali nchini, ikiwa ni pamoja na wabunifu wachanga, wataalamu kutoka vyuoni, wataalamu kutoka Serikalini na Sekta binafsi” Alisema Bw. Doto James

Eneo lingine lililonufaika na msaada huo ni programu ya misitu, ambayo imepatiwa Euro milioni 9.95 kwa lengo la utuzaji wa misitu na uongezaji thamani ya mazao yatokanayo na misitu ili kuongeza kipato kwa Wananchi, kupunguza umasikini na kulinda mazingira.

Katibu Mkuu amemshukuru balozi wa Finland Nchini, Mhe. Pekka Hukka kwa msaada walioutoa na kwa kuunga mkono shughuli za maendeleo za Serikali, na kuongeza kuwa Finland wamekuwa wakifadhili miradi mbalimbali nchini, ukiwemo mradi wa kilimo biashara Mkoani Lindi na Mtwara (LIMAS), uliogharimu Euro milioni 9, Mradi wa kuimarisha usambazaji na upatikanaji wa umeme wa uhakika Jijini Dar es Salaam, uliogharimu Euro milioni 25, na Programu ya maboresho ya Serikali za Mitaa, Euro milioni 10.5

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja aliiishukuru Serikali ya Finland kwa kuendelea kuisaidia Taasisi hiyo.

‘Hii ni mara ya tatu Finland wamekuwa wakitusaidia kuendeleza jitihada zilizoanzishwa na Serikali yetu ambapo awamu ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2012 ambapo walitupatia Euro milioni 7, mwaka 2014 Euro milioni 12 na sasa wametupatia Euro milioni 9.90 huu ni msaada mkubwa’ alisema Profesa Semboja.

Aidha kwa upande wake Balozi wa Finland Bw. Pekka Hukka, aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendeleza ushirikiano na Serikali yake, na kuongeza kuwa msaada huo ni muhimu sana katika kutimiza malengo ya maendeleo ya nchi.

Amesema msaada huo ukitumika ipasavyo hasa katika kuendeleza mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu utasadia kuongeza ajira na kuongeza pato la Taifa.

Ameitaka Serikali kupitia Wizara ya nishati,  kushirikiana na sekta binafsi na kuitumia fursa hiyo ya kuboresha misitu ili kuiongezea nchi mapato zaidi yatakayotokana na makusanyo ya kodi.

Rais Magufuli Ateua Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amteua Bi. Stella Tullo Chagi kuwa Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba wa Wilaya.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Eng. John Kijazi ametangaza kuwa uteuzi huo Bi. Stella Tullo umeanza rasmi toka Novemba 25, 2017. 

Zitto Kabwe Akerwa na Biashara ya Watumwa Inayoendelea Libya.....Aitaka Tanzania isiingie Uwanjani dhidi ya Libya Jumapili

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto Kabwe ameitaka timu ya taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) kutoshuka dimbani kuikabili Libya siku ya Jumapili katika michuano ya CECAFA ikiwa ni hatua ya kuonyesha kuchukizwa na vitendo vya biashara ya utumwa vinavyoendelea katika nchi hiyo.

Zitto ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter ikiwa zimesalia siku chache  kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Bara kucheza mchezo wake wa kwanza siku ya Jumapili ya Desemba 3 dhidi ya Libya katika michuano ya Afrika Mashariki na Kati inayofanyika huko nchini Kenya.

    Leo @masoudkipanya ameshauri Tanzania isusie mechi yake dhidi ya Libya siku ya Jumapili kuonyesha kuchukizwa na Biashara ya Utumwa. Ninaunga mkono. Tanzania isiingie Uwanjani kucheza na Libya. @SADC_News iagize nchi zake zote zirudishe mabalozi wake kutoka Libya.

Kilimanjaro Stars itacheza mchezo huo wa kundi A, katika kuwania kombe la michuano ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA ambayo inatarajiwa kuchezwa nchini Kenya kuanzia Desembe 3 hadi 17 mwaka huu.

Mataifa 10 yanatarajiwa kushiriki katika michuano hiyo mikubwa kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki huku droo ya hatua ya makundi ikionyesha mwenyeji Kenya itacheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Rwanda huku Tanzania ikiikabili Libya siku hiyo.

Rais wa Nigeria atoa neno kuhusu soko la watumwa Libya

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameingilia kati suala ambalo sasa limeigusa dunia nzima kwa kitendo cha raia wa Libya kuwauza kama watumwa wahamiaji wanaoingia nchini humo.

Kwenye ukurasa wake wa twitter Rais Buhari amesema vitendo hivyo havikubaliki, na kwamba wako tayari kufanya lolote kuwalinda raia wake ambao pia ni miongoni mwa wahanga wa biashara hiyo, yenye ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

“Hali ya Libya ya watu kuuzwa ni ya kutisha na haikubaliki, tutafanya kila kitu kuwalinda raia wetu popote walipo, na pia tumeshaanza kuwarudisha nyumbani wanigeria wote waliopo Libya na sehemu nyingine, tutahakikisha wote wanarejea nyumbani salama na kuhudumiwa”, ameandika Rais Buhari.

Kitendo cha raia wa Libya kuwauza wahamiaji wanaoingia nchini humo ambao wengi wao ni raia wa mataifa ya Afrika Magharibi, kimeishtua dunia nzima ambapo mpaka watu maarufu mbali mbali duniani, wamekuwa wakipost kwenye mitandao ya kijamii kukemea vitendo hivyo.

SOIL FOR SECOND YEAR PREPARE YOURSELF














Recent

 
Back To Top
Copyright © 2014 JAMII FOCUS. Designed by OddThemes