Gavana wa Kaunti ya Nyeri nchini Kenya Wahome Gakuru ameaga dunia mapema siku ya Jumanne baada ya kupata ajali mbaya barabarani eneo la Kabati katika barabara kuu ya Thika-Sagana katika kaunti ya Murang’a.
Akizungumzia tukio hilo, Kaunti Kamishna wa Murang’a John Elungata amesema eneo hilo la Kabati ni hatari sana hasa unapokuwa katika mwendo wa kasi.
Maafisa polisi wametoa taarifa ya kuwa gari la Gavana huyo lilikuwa na abiria wanne ambao ni msaidizi wake, mlinzi na dereva huku msaidizi wake akivunjika mguu na mkono lakini Dereva hali yake sio mbaya.
Gavana huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Thika Level 5 kwa matibabu ya haraka lakini ikashindikana. Mwili wa Gavana umesafirishwa katika chumba cha kuhifadhia maiti ya Lee mjini Nairobi.
Hii ni picha ya mwisho aliyopiga Gavana huyo akiwepo shule ya upili ya Alliance Boys:
Post a Comment