Mwanachama wa ACT-Wazalendo Mheshimiwa Zitto Kabwe amefikishwa kituo cha polisi kilichopo Kamata Kariakoo jijini Dar huku jeshi hilo wakikwapua simu yake ili kufanya uchunguzi zaidi.
Hayo yamesemwa na Katibu Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma, Ado Shaibu kuwa wameahidi watairudisha simu ya Mheshimiwa Zitto kesho jioni na kutakiwa kwa mara nyingine kuripoti hapo Novemba 27 mwaka huu.
Aidha, jeshi la Polisi wametoa taarifa kuwa lazima wafike Ofisi za Makao Makuu ya Chama cha ACT-Wazalendo kufanya uchunguzi wa kina kwa kupekua nyaraka zote kuhusiana na takwimu za Serikali.
Post a Comment