BREAKING NEWS

Comments

Saturday, November 11, 2017

MARSEILLE YAMFUKUZA PATRICE EVRA BAADA YA KUMPIGA TEKE SHABIKI


Marseille imetangaza kuwa imemfukuza Patrice Evra klabuni hapo baada ya kumpiga teke shabiki wiki iliyopita.
Kuelekea mechi ya Ligi ya Europa dhidi ya Vitoria Guimaraes, Evra alianza kujibizana na shabiki msafiri kabla ya kumpiga teke kichwani shabiki huyo.
Marseille awali walimsimamisha mchezaji huyo wakati wakiendelea kufanya uchunguzi, lakini uamuzi wa UEFA kumfungia Evra kucheza mechi zote hadi Juni 30 kumechangia mkataba wa mchezaji huyo kusitishwa mara moja.
Evra amejiunga na Marseille mwanzoni mwa 2017, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 akicheza jumla ya mechi 17 baada ya kupewa mkataba wa miezi 18 na miamba hao wa Ufaransa.

Beki huyo wa zamani wa Manchester United bado anaweza kusajiliwa na klabu nyingine kabla ya kumalizika kwa adhabu yake, lakini hataweza kucheza mechi yoyote ya Ligi ya Mabingwa au Ligi ya Europa

Share this:

Post a Comment

 
Back To Top
Copyright © 2014 JAMII FOCUS. Designed by OddThemes