BREAKING NEWS

Comments

Sunday, November 12, 2017

MIKE TYSON AZUILIWA KUINGIA NCHINI CHILE


Bingwa wa uzani mzito duniani Mike Tyson amezuiliwa kuhudhuria sherehe ya kupeana tuzo mjini Santiago, Chile.
Tyson raia wa Marekani mwenye umri wa miaka 51 ambaye aliwahi wakati mmoja kuhudumia kifungo jela kwa ubakaji, unyanyasaji na umiliki wa dawa za kulevya alirudishwa nyumbani na maafisa wa polisi wa idara ya uhamiaji.
Maafisa wa polisi katika Uwanja wa Ndege wa  Santiago walisema kuwa Tyson alirudishwa nyumbani kwa kufeli kuafikia sheria za uhamiaji.
Ikumbukwe kuwa Tyson alizuiliwa kuingia nchini Uingereza 2013 kutokana na matatizo yaliomkuba wakati wa nyuma.
''Baada ya kutathmini rekodi yake kulingana na sheria za uhamiaji, wageni wote ambao walihukumiwa kwa kutekeleza uhalifu wowote hawaruhusiwi kuingia nchini humu,” polisi walisema.
Bingwa huyo mara mbili alihudumia miaka mitata jela katika kifungo cha miaka sita 1992 kwa kumbaka mgombea wa shindano la malkia wa urembo nchini humo.
Alikuwa bingwa wa uzani mzito mwenye umri mdogo katika historia ya uzani huo wakati alipomshinda Trevor Berbick 1986.

Share this:

Post a Comment

 
Back To Top
Copyright © 2014 JAMII FOCUS. Designed by OddThemes