BREAKING NEWS

Comments

Tuesday, November 7, 2017

Nyalandu Amtembelea Lowassa Ofisini Kwake

Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Lazaro Nyalandu amemtembelea Waziri Mkuu wa zamani na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa ofisini kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Nyalandu aliyejiondoa CCM wiki iliyopita leo Jumanne Novemba 7,2017 amemshukuru Lowassa kwa kuonyesha njia kwa wengine kuwa kuna maisha nje ya CCM.

“Mzee wangu nimekuja kujitambulisha na kusema asante kutufungulia mlango,” amesema Nyalandu katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya Lowassa.

Kwa upande wake, Lowassa aliyetoka CCM mwaka 2015 amemkaribisha Nyalandu upinzani akisema, “Nimefarijika kuja huku karibu sana tushirikiane na kwa hakika 2020 tutavuka daraja.”

Share this:

Post a Comment

 
Back To Top
Copyright © 2014 JAMII FOCUS. Designed by OddThemes