Klabu ya Simba imeto taarifa mpya kuhusu mchezaji wao Said Ndemla ambaye alikuwa asafiri leo kwenda Sweden kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa:
Tunapenda kuwafahamisha kuwa safari ya mchezaji wetu Hamis Said Juma Ndemla iliyokuwa ifanyike leo Jumanne imesogezwa mbele.
Ndemla ambaye amepata nafasi ya kwenda kufanya majaribio katika klabu ya AFC Eskilstuna inayoshiriki ligi kuu nchini Sweden ,sasa ataondoka nchini siku ya Alhamis ya tarehe 9 ya mwezi huu.
Mabadiliko haya ya safari hayataathiri muda wake wa majaribio katika klabu hiyo,ambapo atakuwa huko kwa siku 14.
Imetolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano,
Simba Sports Club.
Haji S.Manara.
7/11/2017
Post a Comment