BREAKING NEWS

Comments

Monday, November 13, 2017

Tetemeko laua watu 200 Iraq, Iran


Temetemo la ardhi la ukubwa wa 7.3 katika vipimo vya Richter katika eneo la mpaka wa Iraq na Iran limesababisha vifo vya watu 200 na kuwaacha wengine 1000 wakiwa majeruhi, vyombo vya habari vimeripoti.
Idara ya Jiolojia ya Marekani (USGS) imesema tetemeko kubwa limepiga eneo la Halabjah, kusini mashariki mwa Sulaymaniyah, mji mkuu wa eneo lenye utawala wa ndani la Kurd kaskazini mwa Iraq.
Tetemeko hilo lilizua hofu hadi kusababisha watu kukimbia kutoka ndani ya nyumba wakikimbilia barabarani. Misikiti kwenye mji mkuu wa Iraq, Baghdad imekuwa ikifanya maombi kwa kutumia vipaza sauti.
Wengi wa waathiriwa walikuwa kwenye mji wa Sarpol-e Zahab, kilomita 15 kutoka mpakani. Uharibifu umeripotiwa kuetka katika vijiji vinane kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu nchini Iran Morteza Salim.
Tetemeko hilo ambalo mawimbi yake yalisikika hadi Qatar, Uturuki, Israel na Kuwait lilipiga saa 3:18 usiku kwa saa za Mashariki ya Kati. Mtawanyiko wa mawimbi ulianzia chini umbali wa kilomita 33.9.
Taarifa za awali za shirika la habari la Iran (ISNA) zilisema watu 61 walikufa nawengine 300 walijeruhiwa katika jimbo la Kermanshah kwenye mpaka na Iraq. Lakini idadi ya vifo iliendelea kuongezeka.
Tofauti na Iraq, Iran ni nchi inayokabiliwa na matetemeko ya ardhi. Mwaka 2003, tetemeko la ukubwa wa 6.6 ndilo lilikuwa kubwa zaidi na lilisababisha vifo vya watu 26,000.

Share this:

Post a Comment

 
Back To Top
Copyright © 2014 JAMII FOCUS. Designed by OddThemes